Khalai azungumza na mimea https://storybookscanada.ca/images/0089/02.jpg" alt="A girl in a field waving."/> Khalai ni msichana mwenye umri wa miaka saba. Jina lake lina maana ya ‘aliye mzuri' katika lugha yake ya Lubukusu. https://storybookscanada.ca/images/0089/03.jpg" alt="A girl talking to an orange tree."/> Khalai anaamka na kuongea na mmea mchanga wa Mchungwa, “Tafadhali mti wa Mchungwa, kua mkubwa uzae machungwa mengi mabivu.” https://storybookscanada.ca/images/0089/04.jpg" alt="A girl kneeling on the ground talking to grass."/> Khalai anaenda shuleni na njiani anaongea na Nyasi, “Tafadhali Nyasi, kua kijani zaidi na zaidi na wala usikauke.” https://storybookscanada.ca/images/0089/05.jpg" alt="A girl looking at wild flowers."/> Khalai anayapita Maua ya mwituni na kusema, “Tafadhali Maua, endelea kunawiri ili niweze kukuweka kwenye nywele zangu.” https://storybookscanada.ca/images/0089/06.jpg" alt="A girl next to a tree in a school playground."/> Akiwa shuleni, Khalai anazunguumza na Mti ulioko katikati ya shule, “Tafadhali Mti, toa matawi makubwa ili tusome chini ya kivuli chako.” https://storybookscanada.ca/images/0089/07.jpg" alt="A girl talking to a hedge outside a school."/> Khalai anazunguumza na ua unaoizingira shule yake, “Tafadhali ua, kuwa mwenye nguvu ili uzuie shule yetu kutokana na watu wabaya.” https://storybookscanada.ca/images/0089/08.jpg" alt="A girl next to an orange tree."/> Anaporudi nyumbani alasiri, Khalai anautembelea mti wa Mchungwa kuangalia kama machungwa yameiva. https://storybookscanada.ca/images/0089/09.jpg" alt="A girl next to an orange tree."/> “Machungwa bado mabichi,” Khalai anashusha pumzi. “Nitakuona kesho, we mti wa machungwa. Labda utanipa chungwa bivu wakati huo.”